NANE ZA MOTO LIGI KUU YA NBC.

LIGI Kuu ya NBC itaendelea leo kwa michezo yote nane kupigwa saa 10:00 alasiri ikiwa mbashara katika chaneli mbalimbali za Azam Tv.

Visiwani Zanzibar katika uwanja wa New Amaan itapigwa ‘Dabi’ ya Dar es Salaam kati ya Young Africans itakayokuwa mwenyeji wa Azam.

Mchezo huo ndio mkubwa kwa leo ambapo wababe hao wapo katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC hivyo watazisaka alama tatu muhimu kuhakikisha wanajiweka kwenye nafasi nzuri.

Timu ya Mtibwa Sugar itakuwa mwenyeji wa timu ya Simba katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro ikiwa Simba ipo katika mbio za ubingwa sambamba na Young Africans na Azam hivyo alama tatu zikiwa na maana kubwa ya kuendelea kusalia kwenye kupambania ubingwa.

TRA United itaikaribisha timu ya Coastal Union katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha huku Fountain Gate ikichuana na Mashujaa katika uwanja wa Black Rhino uliopo Karatu, Arusha.

Kwa upande wa Dodoma Jiji itakuwa mwenyeji wa timu ya JKT Tanzania katka uwanja wa Jamhuri Dodoma huku Singida Black Stars ikichuana na Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Airtel, Singida.

Nayo timu ya Pamba Jiji itakutana na timu ya Mbeya City katika uwanja wa CCM Kirumba huku KMC ikichuana na timu ya Namungo katika uwanja wa KMC Complex ambapo KMC tayari imeshuka daraja na hivyo haitakuwa sehemu ya Ligi akuu ya NBC msimu wa 2026/27.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *