VITA YA KISASI ‘DABI’ YA MZIZIMA LEO.

‘Dabi’ ya Mzizima leo inatarajiwa kuwa mchezo wa kuvutia wa Ligi Kuu ya NBC wakati Azam ikiwakaribisha Simba kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar saa 1:00 usiku.

Mchezo huo ni muhimu kwa timu zote ikiwa kila timu inataka alama tatu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC.

Azam iko nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa na alama 14 baada ya michezo sita , ikishinda michezo minne na sare mbili, ikifunga mabao 11 huku ikiruhusu mabao matano.

Simba iko nafasi ya pili ikiwa imecheza michezo mitano na kufanikiwa kushinda michezo yote huku timu hiyo ikifunga mabao tisa na kuruhusu mabao mawili pamoja na kuvuna alama 15.

Hassan Mubiru (kulia) akichuana na mchezaji wa timu ya Namungo.

Hassan Mubiru ni mmoja wa nyota wa kuchungwa kwa timu ya Azam akiwa amefanikiwa kufunga bao moja asisti mbili ikiwa ni ndani ya dakika 265 alizocheza ndani ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027.

Abdul Suleiman nae ni mmoja wa nyota wa kuchungwa akifanikiwa kufunga mabao manne ndani ya dakika 275 ikiwa ni sawa na michezo minne amecheza ndani ya timu ya Azam.

Libasse Gueye

Libasse Gueye ndie mchezaji wa kuchungwa kwa upande wa timu ya Simba akiwa amehusika katika mabao sita kwa kufunga bao moja, assisti tano ndani ya dakika 384 alizocheza kwenye Ligi Kuu ya NBC.

Clatous Chama wa Simba akiwa amefanikiwa kufunga mabao matatu ndani ya michezo minne huku akiwa ametumia dakika 357.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *