‘WANANCHI’ WASHINDA SITA KATI YA SITA LIGI KUU YA NBC.

Timu ya Young Africans imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa ligi Kuu ya NBC uliochezwa katika uwanja wa KMC jijini Dar es saalam.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Oumar Komara dakika ya 55 na likiwapa Yanga alama tatu muhimu.

Hata hivyo mchezo huo ulishuhudia Yanga wakimaliza pungufu baada ya kiungo wao Stephane Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu.

Baada ya matokea hayo Yanga inaendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa na alama 18 ikicheza michezo sita, ikishinda yote sita ,huku ikiwa imefunga mabao 16 na kufungwa mawili pekee.

Geita Gold yenyewe inashika nafasi ya tisa ikiwa na alama 7 baada ya michezo sita, ikiwa imeshinda miwili, sare moja na kupoteza michezo mitatu, imefunga mabao tisa na kufungwa nane.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *