LIGI Kuu ya NBC 2026/2027 imeendelea kushika kasi ikiwa ni mzunguko wa nane ambapo timu ya Coastal Union ya Tanga iliikaribisha timu ya Singida Black Stars katika uwanja wa Mkwakwani Tanga Oktoba 12 majira ya saa 12:00 jioni na kuibuka na ushindi wa bao moja.
Kipindi cha kwanza kilianza kwa kasi huku timu zote mbili zikipambana kupata alama muhimu za mchezo huo na ilichukua dakika 13 kwa Coastal Union kufungua ukurasa wa mabao kupitia Gradi Kiala bao lililodumu hadi timu zinaenda mapumziko.
Kipindi cha pili kilirejea kwa ushindani mkubwa huku Singida Black Stars ikipambana kupata bao la kusawazisha katika mchezo huo ikiwa Coastal Union wakijaribu kuongeza bao la pili, licha ya juhudi hizo kwa timu zote mbili hakuna timu iliyofanikiwa kubadilisha matokeo hivyo mchezo kutamatika kwa timu ya Coastal Union kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Singida.
Mshambuliaji Gradi Kiala wa Coastal Union ndiye alichukua tuzo ya mchezaji bora wa mchezo huo kutokana na ustadi aliouonyesha katika mchezo huo