MZUNGUKO wa nane wa Ligi Kuu ya NBC unaendelea leo jijini Dar es Salaam kwa mchezo mmoja ambapo timu ya Simba itakuwa mwenyeji wa timu ya Mashujaa mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mchezo huo utachezwa majira ya saa moja usiku, ikumbukwe kuwa michezo ya msimu uliopita wa Ligi Kuu ya NBC 2025/2026 Simba ilishinda michezo yote miwili.
Ndani ya msimu huu wa 2026/2027 wa Ligi Kuu ya NBC Simba iliyopo chini ya Kocha Steve Barker imefanikiwa kushinda michezo yote saba na kukusanya alama zote 21 na kuongoza katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.
Kwa upande wa Mashujaa ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC imefanikiwa kucheza michezo saba ushindi mechi nne na kufungwa michezo mitatu huku ikikusanya alama 12