GEITA, FOUNTAIN ZAGAWANA ALAMA LIGI KUU YA NBC.

LIGI Kuu ya NBC imeendelea jana kwa mchezo uliowakutanisha Geita Gold na Fountain Gate mkoani Geita katika uwanja wa Bukombe na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Fountain Gate iliyokuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji Chukwunonye Macdonald aliyefunga kwa mkwaju wa Penati dakika ya 42 na kuipa timu yake matumaini ya kuondoka na ushindi.

Hata hivyo Geita Gold ilirejea mchezoni kipindi cha pili na kusawazisha kupitia kwa Yusuph Muhilu dakika ya 63 akirejesha ushindani katika mchezo huo.

Baada ya bao hilo timu ziliendelea kutafuta bao la ushindi lakini hakuna iliyofanikiwa kuongeza hadi dakika ya 90 na hivyo wababe hao kugawana alama.

Matokeo hayo yanaifanya Geita Gold kupanda kutoka nafasi ya 13 hadi ya 12 ikiwa imefunga mabao 10 na kukusanya alama nane huku Fountain Gate ikiwa ya 16, imefunga mabao matano na kukusanya alama sita kwenye msimamo wa ligi Kuu ya NBC.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *