MCHUANO wa kuwania ufungaji bora katika Ligi ya Championship ya NBC msimu wa 2026/2027 inaendelea kushika kasi huku kila mchezaji akipambana kuhakikisha anafunga na kuisaidia timu yake.
Mshambuliaji Hamdani Ally wa Transit Camp anaongoza orodha hiyo ya wafungaji bora baada ya kuweka nyavuni mabao tisa ndani ya mizunguko nane ambayo timu yake imeshacheza hadi sasa akiwa ametumia dakika 720.
Ramadhani Kalanje wa KMC mwenye mabao nane ndio anaefuatia kwenye kinyang’anyiro hiki akiwa amefanikiwa kufunga mabao nane hadi sasa ndani ya mizunguko nane ya Ligi ya Championship ya NBC akicheza michezo yote na akitumia dakika 667.
Wachezaji watatu wanalingana kwa idadi ya mabao ambao ni Abuidy Khalebi wa Tabora United akitumia dakika 631, Abdulkarim Segeja wa Kigamboni United akitumia dakika 691 na Oscar Paulo wa Tanzania Prison akitumia dakika 609 kila mmoja akiwa amefanikiwa kufunga mabao sita.
Ushindani huo unaifanya safari ya kuwania tuzo ya mfungaji bora kuwa ya kuvutia, huku kila mchezo ukiwa na nafasi ya kubadilisha mwenendo wa orodha hiyo.
Kwa upande mwingine, uwepo wa wachezaji watatu wenye mabao sita unaongeza ushindani katika nafasi za juu, huku wakisaka kuongeza idadi ya mabao yao katika michezo inayofuata.
Kadri ligi inavyoendelea, macho na matarajio ya mashabiki yataendelea kuelekezwa kwa washambuliaji hao, ambao wanapambana kuandika historia na kutwaa tuzo ya ufungaji bora wa NBC Championship msimu wa 2026/2027.