GUEYE HAKAMATIKI KWENYE SUALA LA KUPIKA MABAO LIGI KUU NBC.

Kiungo wa Simba SC, Libasse Gueye, anaendelea kung’ara katika Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027, akiongoza orodha ya wachezaji wenye pasi nyingi za mwisho zilizozaa mabao (assists), akiwa amefikisha jumla ya pasi saba za mabao.

Gueye amekuwa miongoni mwa wachezaji wanaoonyesha ubora mkubwa katika kutengeneza nafasi za kufunga, akionyesha uwezo wa kulitazama vizuri lango la wapinzani na kuwaunganisha washambuliaji wa timu ya Simba ili waweze kupata mabao na kuiweka katika nafasi nzuri timu hiyo.

Kiungo huyo ametumia dakika 763 ndani ya michezo 10 kuhakikisha anapata hizo pasi saba.

Hussein Zakouani wa Young Africans anashika nafasi ya pili akiwa amefikisha pasi saidizi nne akitumia dakika 443 na michezo nane kuhakikisha anaonyesha ubora wake.

Ki Aziz wa Young Africans nae hayuko mbali amefanikiwa kuweka pasi saidizi tatu mapaka sasa akitumia dakika 224 ndani ya michezo minne.

Harun Chanongo wa timu ya Mashujaa ameweza kutoa pasi saidizi tatu akitumia dakika 289 ndani ya michezo sita.

Ani Elijah wa TRA United naye hayuko mbali ameweka pasi saidizi tatu akitumia dakika 567 ndani ya michezo tisa.

Rashid Chambo wa timu ya Namungo ameonyesha ubora wake katika kutoa pasi saidizi akitumia dakika 568 ndani ya michezo tisa.

Jeancy Mboma wa timu ya Singida Black Stars yupo vizuri akitumia dakika 752 kupata pasi tatu ndani ya msimu wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027 hadi sasa.

Maxi Nzengeli, wa timu ya Young Africans ametumia dakika 881 ndani ya michezo 10 kutoa pasi saidizi tatu.

Kwa Gueye, kuongoza kwa tofauti ya pasi saidizi tatu dhidi ya anayemfuata ni ishara ya mchango wake mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya timu ya Simba.

Hata hivyo, safari ya Ligi Kuu ya NBC bado ni ndefu na ushindani wa kuwania nafasi ya kinara wa ‘assists’ bado unaendelea.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *