KASONGO AWAITA MADAKTARI VIWANJANI

AFISA Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, Almasi Kasongo ameushauri uongozi wa Chama cha Madaktari wa Michezo nchini (TASMA) kutengeneza mazingira rafiki yatakayovutia madaktari wengi zaidi wanaofanya kazi katika Hospitali mbalimbali.

Amesema hayo alipokuwa akifungua Semina ya madaktari wa michezo inayofanyika Mkoani Dar es Salaam kwenye ukumbi wa mikutano katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Tufungue milango ili tuwape nafasi madaktari wanaohudumu katika hospitali zetu ili waweze kuingia kwenye mpira wa miguu kupitia Chama hiki lengo ikiwa kuwapa nafasi ya kuhudumia wachezaji na mashabiki wanaohudhuria viwanjani” amesema Kasongo.

Aidha Kasongo amesisitiza klabu zinazoshiriki Ligi zote msimu ujao kusimamia vizuri eneo la tiba na afya kwani ni eneo muhimu katika utekelezaji wa masharti ya leseni za klabu.

“Ni muhimu klabu zote kuwa na wataalamu wa afya wenye ubobezi, utaalamu na uzoefu wa kutosha kazini ili michezo ichezwe katika hali ya usalama kwani hakuna timu itakayoshiriki mashindano ya msimu ujao bila kuwa na mtaalamu wa afya aliekidhi vigezo vyote” aliongeza Kasongo.

Mafunzo hayo ya ngazi ya juu kwa madaktari wa michezo yaliyoandaliwa na TASMA yatafanyika kwa siku saba lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo maradufu madaktari hao katika matibabu ya wachezaji na mashabiki viwanjani.

2 comments

  1. Hili niliwahi waza na kutamani muda mrefu Sana huu ndo wakati wake, nadhani ni vizuri kukawa na utaratibu wa kuomba online hii kozi ili fursa iwe kwa wote around Tanzania nzima na sio manufaa yawe kwa wanaoishi Dsm pekee.

  2. Pingback: best writing paper

Join the Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *