MICHEZO miwili ya mzunguko wa 18 ya Ligi ya NBC Championship imechezwa leo na michezo yote kumalizika kwa sare.
Mchezo wa kwanza ulizikutanisha Polisi Tanzania dhidi ya Green Warriors saa 8:00 mchana kwenye uwanja wa ushirika, Kilimanjaro na kumalizika kwa suluhu.
Saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro FGA Talents ikaikaribisha Transit Camp na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2 .
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa michezo mitatu kupigwa Mbuni itawakabili Pan African, Pamba dhidi ya Stand United na Mbeya City dhidi ya Mbeya Kwanza.