LIGI ya NBC Championship imeendelea leo Januari 21 kwa michezo mitatu kupigwa kwenye mikoa mitatu tofauti.
Mchezo wa mapema saa 8:00 mchana ulizikutanisha TMA dhidi ya Cosmopolitan kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Mkoani Mwanza Copco ikawakaribisha Biashara United kwenye uwanja wa CCM Kirumba saa 10:00 alasiri na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mchezo wa mwisho kwa leo ulizikutanisha KenGold dhidi ya Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya na kumalizika kwa KenGold kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Ushindi wa KenGold unairejesha kwenye uongozi wa msimamo wa Ligi ya NBC Championship baada ya kufikisha alama 42 kwenye michezo 18.