HAWA HAPA VINARA WA MABAO NBC CHAMPIONSHIP.

 

Jumla ya mabao 329 yameshafungwa katika michezo 144 sawa na mizunguko 18 ya Ligi ya NBC Championship mpaka kufikia sasa.

Edger William wa KenGold ndiye kinara wa upachikaji mabao ndani ya Ligi ya NBC Championship akifunga mabao 15 huku timu yake ikifunga mabao 32.

Boban Bogere wa Biashara United ndiye anayefuatia akifunga mabao 13 kwenye mabao 32 yaliyofungwa na timu yake.

Ramadhani kapera aliyekuwa Mbeya Kwanza kabla ya kutimkia Geita Gold inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC na Salim Aiyee aliyekuwa timu ya Mbuni kabla ya kujiunga na Coastal Union ya Ligi Kuu ya NBC wanafuata kila mmoja akifunga mabao 9.

One comment

  1. Yanga wasipo hudhuria mchezo maarufu wa daby ya kariakoo washushwe tu dalaja au kufungiwa kwenye lig

Join the Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *