Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini(TFF) katika kikao chake cha Agosti 1, 2024 ilijadili nakufanyia maamuzi maoni ya maboresho ya Kanuni za Ligikwa ajili ya toleo la 2024.
Kanuni zilizofanyiwa maboresho na kupitishwa katikakikao hicho ni pamoja na Kanuni ya 7 ya First League kuhusu Nane Bora na Kanuni 7 (saba) za Ligi Kuu ambazoni Kanuni ya 9 kuhusu uwanja, Kanuni ya 17 kuhusuTaratibu za Mchezo, Kanuni ya 31 kuhusu KutofikaUwanjani, Kanuni ya 47 kuhusu Udhibiti kwa Klabu, Kanuni ya 62 kuhusu Wachezaji wa Kigeni, Kanuni ya 77 kuhusu Makocha na Kanuni ya 79 kuhusu MaamuziYasiyokatiwa Rufaa.
Aidha kamati hiyo ilipitisha kanuni mpya 12 ambazozitajumuishwa kwenye toleo la 2024.
Maboresho yote ya Kanuni za Ligi Kuu yaliyoainishwakwenye jedwali hapa chini, yataathiri Kanuni za mashindano mengine yaliyo chini ya TFF na machapishoyake yatatangazwa.
Bonyeza kiunganishi (Link) hapo chini kusoma maboresho hayo.
Suala la ushirikina limezidi sana Kwa maoni yangu kama itawezekana atakae bainika timu ikatwe pointi na faini itakayopitishwa. Na pia waamuzi wawewanahojiwa nao haiwezekani wanatoa maamuzi ya ovyo kweli kweli.
ππππ ππβππ π βππ ππππ’π πππ π£ππππππ§π πππππ π€πππ π‘πππ’ π§ππ ππ€πππ¦π πππππππππ ππ’πππππππ ππ ππππ’ππ’ π πππ βπππ π‘π’πππ‘π π€ππ‘π’ πππππ π€ππ‘πππ’π€π ππ π’π€πππππ π€π πππππ πππππ π€ππππππ βππ€ππ€ππ§ ππ ππ‘ ππ’ππππ’ππ§π ππβπ π§π π€πππ§ππ‘π’ βππ€ππ€ππ§π ππ€π ππππππ§π π¦π π‘πππ’ π§ππ π§π π¦ππππ ππ π ππππ
NI MWENYEKTI WA KAMATI YA LIGI
Hongera sana kwa kazi
Vizuri na asante sana kwa kazi nzuri ya maboresho mnayoifanya kill mala, length ni kujenga kuendana na mahitaji kwa wakati unaofaa. Asanteni sana!
Congratulations for all of you TFF
Kwa mtazamo wangu hapo ni kwamba kama kunamtu atabainika amekiuka sheria imefika sasa wakati mamalaka za soccer kufanya kazi yao kuhakikisha wanatoa adhabu stahiki kwa kila atakae kiuka sheria kwa sababu ukiukwaji wa sheria umekithiri na hili kama tukilifumbia macho naimani kuna wakati litajirufia tena
Mie nashauri kuwa endapo timu yoyote inayoshiriki michezo ya mpira wa miguu itafanya kosa lolote la kikanuni lisisababishe timu pinzani kususia kucheza mchezo husika. Mechi inayokusudiwa lazima ichezwe na baada ya mechi, timu yenye ulalamishi itawasilisha malalamiko yake kwa Bodi kwa maandishi baada ya mchezo ili timu itakayokuwa imefanya makosa iadhibiwe. Sawa kabisa na jinsi inavyofanyika iwapo timu itamchezesha mchezaji ambaye hajasajiliwa.Labda, endapo kosa lililofanyika linaashiria hatari ya usalama au litasababisha timu pinzani isiweze kucheza kwa sababu za kukosa wachezaji au kushindwa kusafiri au kutokujuwa ni uwanja upi utatumika au ikazuiliwa kuingia uwanjani siku ya mechi na mengineyo. Na ni lazima yawekwe wazi kwa maandishi kabla ya kuacha kushiriki mchezo ili bodi iridhie.
Mimi maoni yangu ili ligi iweze kuwa na ushindani haitakiwi mdhamini kudhamini club zaidi ya Moja yaani kuwekeza
Mabo ya GSM kudhamini timu zaidi ya moja na hili mliangalie
Mabo ya GSM kudhamini timu zaidi ya moja na hili mliangalie maana haiwezekani timu zenye rogo ya GSM Fulani anajichukulia matokeo tu