Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini(TFF) katika kikao chake cha Agosti 1, 2024 ilijadili nakufanyia maamuzi maoni ya maboresho ya Kanuni za Ligikwa ajili ya toleo la 2024.
Kanuni zilizofanyiwa maboresho na kupitishwa katikakikao hicho ni pamoja na Kanuni ya 7 ya First League kuhusu Nane Bora na Kanuni 7 (saba) za Ligi Kuu ambazoni Kanuni ya 9 kuhusu uwanja, Kanuni ya 17 kuhusuTaratibu za Mchezo, Kanuni ya 31 kuhusu KutofikaUwanjani, Kanuni ya 47 kuhusu Udhibiti kwa Klabu, Kanuni ya 62 kuhusu Wachezaji wa Kigeni, Kanuni ya 77 kuhusu Makocha na Kanuni ya 79 kuhusu MaamuziYasiyokatiwa Rufaa.
Aidha kamati hiyo ilipitisha kanuni mpya 12 ambazozitajumuishwa kwenye toleo la 2024.
Maboresho yote ya Kanuni za Ligi Kuu yaliyoainishwakwenye jedwali hapa chini, yataathiri Kanuni za mashindano mengine yaliyo chini ya TFF na machapishoyake yatatangazwa.
Bonyeza kiunganishi (Link) hapo chini kusoma maboresho hayo.
Suala la ushirikina limezidi sana Kwa maoni yangu kama itawezekana atakae bainika timu ikatwe pointi na faini itakayopitishwa. Na pia waamuzi wawewanahojiwa nao haiwezekani wanatoa maamuzi ya ovyo kweli kweli.