Author: Yahaya Abushehe

KENGOLD KUENDELEA KUJICHIMBIA KILELENI NBC CHAMPIONSHIP LEO ?

 

NBC Championship mzunguko wa 21 unaanza Leo kwa michezo miwili kupigwa kwenye kwenye mikoa miwili ya Pwani na Morogoro.

Mkoani Pwani Pan African itaikabili KenGold saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Mabatini, KenGold inaongoza msimamo wa Ligi ikiwa na alama 44 kwenye michezo 20 iliyocheza mzunguko huu unaweza kuamua ni nani atakayeongoza usukani wa msimamo wa NBC championship kutokana na alama za timu zinazofuatia, Hivyo ushindi kwenye mchezo huu utamhakikishia kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo.

Mchezo mwengine mkoani Morogoro Transit Camp itaialika Copco kwenye uwanja wa Jamhuri saa 10:00 alasiri, Transit Camp ipo nafasi ya 13 kwenye msimamo ikiwa na alama 19 huku Copco ikiwa nafasi ya 15 ikiwa na alama 13 hivyo kila timu ikiwa na uhitaji wa alama kujinasua kwenye nafasi iliyopo.

YANGA KUIVAA MASHUJAA LIGI KUU YA NBC LEO.

 

LIGI Kuu ya NBC inaendelea Leo Februari 8 kwa mchezo mmoja Kati ya Yanga dhidi ya Mashujaa kwenye uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku.

Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na kumbukumbu ya ushindi kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Dodoma Jiji huku Mashujaa ikipoteza kwenye mchezo wao dhidi ya Simba.

Yanga ipo kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 34 kwenye michezo 13 huku Mashujaa ikiwa nafasi ya 15 kwenye mstari wa kushuka daraja na alama zake tisa kwenye michezo 13.

NBC CHAMPIONSHIP YAPAMBA MOTO.

 

MZUNGUKO wa 20 ligi ya NBC Championship umemalizika na kushuhudia jumla ya michezo nane ikichezwa huku mabao 22 yakifungwa.

KenGold inaendelea kusalia kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 43 kwenye michezo 20 huku Pamba na Biashara United zikifuatia zikiwa na alama 43 kila moja zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

Ruvu Shooting yenye maskani yake mkoani Dodoma kwasasa inaendelea kuburuza mkia kwenye msimamo ikiwa na alama nne pekee kwenye michezo 20 iliyocheza ikifunga mabao nane na kufungwa 41.

LIGI KUU YA NBC KUENDELEA LEO, MASHUJAA KUJIULIZA KWA SIMBA.

 

LIGI Kuu ya NBC inaendelea leo Februari 3 kwa mchezo mmoja kupigwa mkoani Kigoma.

Mashujaa itaikaribisha Simba kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma saa 10:00 alasiri.

Mashujaa inaingia kwenye mchezo huu ikiwa nafasi ya 15 kwenye msimamo ikijikusanyia alama tisa kwenye michezo 12 huku Simba ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na alama 23 kwenye michezo 10.

NBC CHAMPIONSHIP KUPIGWA MIKOA SITA LEO.

 

LIGI ya NBC Championship mzunguko wa 20 unaanza leo Februari 3 kwa michezo sita kupigwa kwenye mikoa sita tofauti.

Mchezo wa mapema saa 8:00 mchana utazikutanisha Stand United dhidi Biashara United kwenye uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga.

Mkoani Mbeya KenGold itaikaribisha Mbeya City saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Sokoine huku KenGold ikiingia kwenye mchezo huu ikiwa kinara kwenye msimamo na alama 43 kwenye michezo 19 huku Mbeya City ikiwa nafasi ya 7 na alama 32 kwenye michezo 19.

Mkoani Arusha ni “ Derby ya Jeshi” kati ya Mbuni na TMA saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid huku alama moja pekee ikiweka utofauti baina ya timu hizi TMA ikiwa nafasi ya nne na Alama 37 huku Mbuni ikiwa nafasi ya tano na alama 36 hivyo kuufanya mchezo huu kuwa wa kuvutia.

Mchezo mwengine utazikutanisha FGA Talents dhidi ya Polisi Tanzania saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Mkoani Mwanza Copco itaikabili Pamba kwenye uwanja wa Nyamagana saa 10:00 alasiri mchezo huu ukiwa ‘Mwanza Derby’ kutokana na timu zote kutokea mkoa wa Mwanza.

Mchezo wa mwisho utapigwa mkoani Pwani Pan African itaikabili Cosmopolitan kwenye uwanja wa Mabatini saa 10:00 alasiri.