Author: Yahaya Abushehe

HAZIJAPOTEZA MCHEZO WOWOTE NYUMBANI NBC CHAMPIONSHIP.

 

JUMLA ya mizunguko 17 sawa na michezo 136 ya Ligi ya NBC Championship tayari imeshachezwa na kushuhudia jumla ya mabao 302 yakifungwa mpaka sasa.

KenGold, Pamba, Mbeya kwanza na TMA ndiyo timu pekee ambazo hazijapoteza mchezo wowote wa nyumbani ndani ya Ligi ya NBC Championship mpaka kufikia hivi sasa.

Pamba,Mbeya Kwanza na TMA zimecheza michezo nane katika viwanja vyao vya nyumbani bila kufungwa huku KenGold ikicheza michezo saba pekee bila kufungwa.

Ruvu Shooting ndiyo timu iliyopoteza michezo mingi zaidi nyumbani baada ya kufungwa jumla ya michezo nane kwenye michezo 10 iliyocheza ndani ya uwanja wake wa nyumbani.

MZUNGUKO WA 17 NBC CHAMPIONSHIP WATAMATIKA, KENGOLD KINARA.

 

MZUNGUKO wa 17 wa Ligi ya NBC Championship umetamatika jana Januari 14 kwa michezo nane kupigwa na jumla ya mabao 16 kufungwa kwa mzunguko huo pekee.

KenGold inaendelea kushikilia usukani wa Ligi hiyo baada ya kufikisha jumla ya alama 39 kwenye michezo 17 huku ikifunga mabao 30 na kuruhusu kufungwa mabao 10.

Ruvu Shooting hali si shwari ikiendelea kuburuza mkia ikiwa na alama tatu pekee baada ya michezo 17 iliyocheza.

MECHI TATU NBC CHAMPIONSHIP KUPIGWA LEO, ZOTE MUBASHARA TV3.

LIGI ya NBC Championship inaendelea hii leo kwa michezo mitatu kupigwa huku yote ikionyeshwa mubashara kupitia TV3.

Mapema saa 8:00 Mchana Stand united itaikaribisha Mbuni kwenye uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga.

Mkoani Mtwara Mbeya kwanza itakuwa mwenyeji wa FGA talents kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona saa 10:00 alasiri na kuoneshwa Live kupitia ST BONGO

Mchezo wa mwisho utapigwa Saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Mabatini mkoani Pwani ambapo Pan Africans itakuwa mwenyeji wa Pamba.

Hii ndio michezo ya mwisho kukamilisha mzunguko wa 17 wa Ligi ya NBC Championship.

KENGOLD YAJIKITA KILELENI NBC CHAMPIONSHIP, RUVU, POLISI HAKUNA MBABE.

 

KENGOLD imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi ya NBC Championship baada ya leo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Green Warriors na kufikisha jumla ya alama 39 kwenye michezo 17.

Ruvu Shooting imelazimishwa suluhu na Polisi Tanzania mchezo uliochezwa uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma saa 10:00 alasiri.

Transit ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani Jamhuri, Morogoro ikakubali kichapo cha bao 1-0 dakika ya mwisho kabisa ya mchezo dhidi ya Mbeya City.

NBC CHAMPIONSHIP HAKUNA KULALA MICHEZO MITATU KUPIGWA LEO.

 

LIGI ya NBC Championship inaendelea leo kwa michezo mitatu kupigwa kwenye mikoa mitatu tofauti.

Green Warriors itaikabili KenGold vinara wa NBC Championship saa 8:00 mchana kwenye uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.

Ruvu Shooting itaikaribisha Polisi Tanzania saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Mchezo wa mwisho utakuwa kati ya Transit Camp na Mbeya City saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.