CHAMA KINARA WA MABAO YA GUU LA KULIA LIGI KUU YA NBC.

Kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba na raia wa Zambia, Clatous Chama, anaongoza orodha ya wachezaji waliofunga mabao mengi kwa kutumia mguu wa kulia katika msimu wa 2026/27 wa Ligi Kuu ya NBC hadi sasa, akiwa amefunga mabao manne ndani mizunguko nane ya ligi hiyo.

Chama anaendelea kuonyesha uwezo wake wa kutumia mguu wa kulia katika kumalizia mashambulizi, akiwazidi wachezaji wengine wanaofuatia katika orodha hiyo ambao kila mmoja amefunga mabao matatu.

Wachezaji hao ni Maxi Nzengeli (Young Africans), Herbet Lukindo (Namungo), Maabad Maabad (Coastal Union), Abdul Suleiman (Azam) na Anuary Jabir (Polisi Tanzania), ambao wanashika nafasi zinazofuata kwa kufunga mabao matatu kila mmoja kwa kutumia mguu wa kulia.

Ushindani huo unaonyesha namna wachezaji ndani ya Ligi Kuu ya NBC wanavyotumia uwezo wao wa kiufundi na umaliziaji katika kutikisa nyavu za wapinzani wao na kusaidia timu zao kufikia malengo waliyojiwekea katika ligi hiyo.

Kwa Chama kuongoza orodha hii ni ishara nyingine ya mchango wake katika safu ya ushambuliaji ya timu ya Simba ambayo inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya NBC akiwa na alama 24 baada ya kushinda michezo yote nane hadi sasa, huku ushindani ukiendelea kuwa mkali kadiri ladha za Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/27 zinavyoendelea kuwa tamu.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *