FIRST LEAGUE, KUNDI A KWA MOTO MSIMU HUU.

 

Mzunguko wa tatu wa First League umetamatika kwa michezo nane ambapo kundi A ni michezo minne na B ni michezo minne kwa mzunguko mmoja.

Kinara wa Kundi A ni Cosmopolitan akiwa amecheza michezo mitatu ushindi mbili na kufungwa mchezo mmoja huku timu hiyo ikifunga mabao matano na kufungwa mabao mawili na kukusanya alama sita.

Nyumbu nao hawapo mbali wakiwa nafasi ya pili ikiwa na michezo mitatu, ushindi mbili, kufungwa moja, kufunga mabao matano na kuruhusu matatu huku ikiwa na alama sita.

Magnet ipo nafasi ya tatu kwenye kundi A ikiwa imeshinda michezo miwili, kufungwa mmoja, kuweka nyavuni mabao manne na kufungwa mabao manne huku ikiwa na alama sita.

Hausang ya Njombe imecheza michezo mitatu, ikishinda mchezo mmoja, sare mbili na kufunga mabao mawili huku ikiruhusu bao moja, aidha timu hiyo imekusanya alama tano.

Moro Kids ya Morogoro imecheza michezo mitatu ushindi moja, sare mbili na kufunga bao moja bila kuruhusu bao lolote huku ikikusanya alama tano.

Pan African ipo nafasi ya sita katika msimamo wa kundi A ikiwa imecheza michezo mitatu, ushindi mchezo mmoja, na kufungwa michezo miwili huku ikifunga mabao mawili na kuruhusu mabao matano huku ikikusanya alama tatu.

Nafasi ya saba ipo timu ya Dar City ikiwa imecheza michezo mitatu, sare mbili na kufungwa mchezo mmoja aidha imefunga bao moja na kuruhusu mabao mawili huku ikikusanya alama mbili.

Barberian iliyoshuka daraja kutoka Ligi ya Championship ya NBC inashika nafasi ya nane kwenye mshimamo wa kundi A ikiwa imecheza michezo mitatu na kufungwa michezo yote huku ikiwa haijapata bao lolote na kuruhusu mabao matatu ikiwa haina alama yoyote.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *