GEITA, STAND VITA YA NAFASI NBC CHAMPIONSHIP LEO.

 

Ligi ya Championship ya NBC inaendelea leo Januari 12, 2025 kwa michezo miwili kuchezwa katika mikoa ya Geita na Pwani.

Mchezo wa kwanza utazikutanisha Kiluvya iliyo nafasi pili kutoka mwisho dhidi ya Mtibwa Sugar vinara wa Ligi ya Championship ya NBC katika uwanja wa Mabatini mkoani Pwani kuanzia saa 10:00 alasiri.

Mchezo wa pili utazikutanisha Geita Gold yenye alama 30 dhidi ya Stand United yenye alama 29 kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC.

Mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa 10:00 alasiri na unatazamiwa kuwa mchezo wenye ushindani mkali kutokana na alama za kila timu kwenye msimamo, ambapo timu mshindi wa mchezo huu itajihakikishia nafasi ya tatu kwenye msimamo.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho Januari 13, 2024 kwa mchezo mmoja wa kuhitimisha mzunguko wa 15 kati ya Transit Camp na African Sports saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Mabatini, Pwani.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *