MBIO za mafanikio ya timu ndani ya msimu wa 2026/2027 wa Ligi Kuu ya NBC zinanogeshwa na uwezo wa mabeki wa timu mbalimbali kuhusika katika mabao na sio kuzuia pekee.
Hawa hapa wakali wa kutoa pasi saidizi za mabao kwa timu zao msimu huu hadi sasa;
Salum Khamis wa JKT Tanzania anaongoza kwa pasi saidizi mbili akiwa ametumia dakika 491 ndani ya michezo nane ya Ligi Kuu ya NBC.
Chadrack Boka wa timu ya Young Africans amefanikiwa kuweka pasi saidizi mbili ndani ya dakika 527 za mechi saba msimu huu.
Nathaniel Chilambo wa timu ya Simba amecheza michezo 10 akitumia dakika 844 amefanikiwa kupata pasi saidizi za mabao mbili.
Denis Mushi wa Polisi Tanzania amecheza michezo 11 sawa na dakika 981.
Martin Kigi wa Geita Gold ametumia dakika 990 kutoa pasi saidizi mbili ndani ya michezo 11 ya Ligi Kuu ya NBC.
Wachezaji wote hawa wametoa pasi saidizi sawa (2) na tofauti yao ikiwa kwenye dakika walizocheza ambapo Salum Khamis amekuwa kinara kwa kutoa pasi hizo katika dakika chache zaidi ya wenzake.