LIGI Kuu ya NBC inaendelea kwa mzunguko wa 17 huku mechi nne zikichezwa katika viwanja mbalimbali nchini kuanzia majira ya saa nane mchana.
Mchezo wa kwanza utachezwa saa nane mchana katika uwanja wa Jamhuri Dodoma ambapo Dodoma Jiji watawakaribisha Pamba Jiji kutoka jijini Mwanza .
Sambamba na mchezo huo Tanzania Prisons “wajelajela” watawakaribisha timu ya Mashujaa “Wana mapigo na mwendo” katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya muda ikiwa ni saa nane mchana.
Mchezo wa tatu kwa siku ya leo ni timu ya Fountain Gate watawakaribisha timu ya Simba katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo Babati Mkoani Manyara saa kumi alasiri.
Mkoani Dar es Salaam wenyeji wa uwanja wa Chamazi timu ya Azam watawakaribisha timu ya KMC “Kinoboys” katika mchezo utakaochezwa saa moja jioni.