Ligi Kuu ya NBC inafika tamati Leo Mei 28 kwa michezo nane ikihusisha timu zote 16 Zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC kupigwa kuanzia saa 10:00 alasiri kwenye mikoa saba tofauti.
Michezo ya leo itaamua hatma ya baadhi ya timu ikiwemo vita ya nafasi ya pili, nani kushuka daraja, nani kucheza mtoano (Playoff) na vita ya ufungaji bora.
Nafasi ya pili inapambaniwa na Timu za Azam na Simba ambapo Azam Ina alama 66 kwenye michezo 29 sawa Simba wakitofautiana kwenye mabao ya kufunga na kufungwa ambapo Azam akiwa na utofauti mkubwa wa mabao (40) kuizidi Simba (32).
Anayeshika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya NBC anapata nafasi ya kuiwakilisha Nchi kwenye michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika.
Vita ya kushuka daraja na Kuungana na Mtibwa Sugar iliyotangualia Ligi ya NBC ya Championship ipo mikononi mwa Geita Gold na Tabora United ambapo Geita ikiwa na alama 25 huku Tabora United ikiwa na alama 27.
Geita inahitaji ushindi na kuomba Tabora ipoteze ili kufikisha alama 28 ambazo zitaipa nafasi ya kushiriki hatua ya mtoano (Playoff) , Tabora inahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kucheza mtoano (Playoff).
Kila nafasi ambayo timu itamaliza kwenye Ligi Kuu ya NBC ina zawadi ya fedha kutoka kwa mdhamini mwenye haki ya matangazo ya Ligi Kuu ya NBC Azam Tv.
Hongereni sana kwa kuendelea kufanya kazi nzuri.Ligi ya NBC kwa msimu huu imekwisha vizuri japo kwa dosari ndogo.Ligi ilianza kukiwa bado kuna matatizo ya usajili kwa baadhi ya vilabu shiriki.Tabora United ilicheza pungufu dhidi ya Azam na mchezo hauukuisha.Matokeo ya pointi tatu na magoli manne yalibaki.Saidieni Jambo kama hili halijirudii.
Nashauri mnapowaondolea watu status za VVIP ni wema mkawajulisha rasmi kuliko kukaa kimya.Sitaki kuamini kuwa nimeondolewa status hiyo.Mpaka sasa bado nasubiri kujibiwa ombi la kupatiwa mwaliko wa kuangalia mechi za msimu ulioisha licha ya picha zangu kupokelewa na ofisi yenu.Kawaida karamu usiyo alikuwa ukivunja kikombe utalalipa.Sikufika kuona michezo mingi ya ligi ya Msimu ulioisha.
Ratiba zipangwe kwa mazingira halisi ya nchi yetu.
Makosa ya kibinadamu yasiwe kwa marefa tu yaonekane pia kwa wachezaji.Marefa wanawake wanafanya vizuri sana waendelee kuwa encouraged.Mwisho nashauri kila MTU atimize wajibu wake ktk nafasi yake bila kusimamiwa.Watendaji wa Bodi wajenge nidhamu ya kusikiliza watu kama ilivyo kwa viongozi wa juu Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu. Uhuru wa timu kuchagua viwanja vya nyumbani uwe na ukomo,sio kila timu inapojisikia ifanye hivyo mabadiliko yasiyo tija huleta kichefuchefu.Wadhamini mbambali wajue mipaka yao wasiruhusiwe kwenda mpaka jikoni kama ilivyo kwa wanasiasa.Je Bahati ilipopewa nafasi ya kuandaa fainali na kunyimwa haikuwa dosari mbaya ktk mpira wetu? Mwisho jitahidi kuzuia kamati kuingia mpirani kwa nguvu zenu zote kutunza heshima yenu na mpira wetu.Tumeieni hata wachunguzi binafsi wabobevu ktk eneo hili.Mlipokeaji kauli ya Tembo Harmonize kwa Aziz Ki kufunga hatrick ktk mchezo wa mwisho na kumshinda Fei Toto ktk Kiatu cha mfungaji bora? Kauli hii ilitolewa kabla ya mchezo na ikawa hivyo.Hali kama hiyo iwafungue macho yanaendelea nje ya macho yenu.
Hongereni sana kwa kuheshimisha mpira wetu na kwa wasaidizi wenu wachache wasiowasaidia wapeni nafasi ya kubadilika.Ahsate
Bahati/Bahati Manyara
ok
nice