LIGI KUU YA NBC RASMI AGOSTI 16.

 

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imetangaza tarehe ya kuanza kwa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025 kuwa ni Agosti 16, 2024.

Kalenda ya matukio iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inaonyesha kuwa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025 itamalizika Mei 24,2025.

Taarifa hiyo imeeleza tarehe ya kuanza na kumalizika kwa Ligi za NBC Championship na Ligi ya First League msimu wa 2024/2025.

NBC Championship inatarajiwa kuanza Septemba 14, 2024 na kutamatika Mei 10, 2025 huku First League ikitarajiwa kuanza Novemba 23, 2024 na kutamatika Aprili 19, 2025.

One comment

  1. Sawa kalenda imetajwa lakn mbna ratiba za mechi hakuna au tarehe 16 ztacheza mbingu na ardhi?

Join the Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *