PAZIA LA LIGI KUU YA NBC MSIMU WA 2025/2026 KUFUNGULIWA LEO.

PAZIA la Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026 linafunguliwa leo kwa michezo miwili kuchezwa kwenye viwanja vya KMC, Dar es salaam na Mkwakwani, Tanga.

Mchezo wa Kwanza kwenye uwanja wa KMC Complex utazikutanisha timu za KMC ya Dar es salaam na Dodoma Jiji ya Dodoma.

 

 

KMC COMPLEX – DAR ES SALAAM

 

 

Wakizungumza Kuelekea mchezo huo makocha na wachezaji wa timu zote mbili wameonesha kuwa tayari kwa mchezo huo huku wakiwa na shauku kubwa baada ya kuwa timu za kwanza kucheza kwa msimu wa 2025/26.

 

 

msimu wa 2025/2026

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kwa upande wa KMC waliwakilishwa na Kocha Mkuu Marcio Maximo na Mchezaji Daruweshi Saliboko huku Dodoma Jiji wakiwakilishwa na Kocha Mkuu Vincent Mashami na Nahodha Augustino Nsata.

Mchezo wa pili utapigwa saa 1:00 usiku kati ya Coastal Union na Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga ambapo Coastal Union ilimaliza msimu wa 2024/2025 ikiwa nafasi ya nane huku Dodoma Jiji ikimaliza nafasi 12.

One comment

  1. Naitwa
    ASANTE Dogo mshauli
    Ni musanii chipukizi toka NGARA KAGERA TANZANIA
    piya ni shabiki wa timu ya
    SIMBA SPORT CLB
    Mwaka hu wana simba tuombe mungu na tuendelee kujipa imani ira kikubwa KOCHA Ange badili mbinu YONG siyo ya kubec kombe misimu 4 KOCHA AJITAHIDI.

Join the Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *