TIMU ya Mtibwa Sugar imepanda rasmi Ligi Kuu ya NBC ambayo ni Ligi namba nne kwa ubora barani Afrika wakitokea Ligi ya Championship ya NBC baada ya kufanikiwa kufikisha alama 67 ambazo hakuna timu itaweza kuzifikia katika michezo 28 abayo timu hiyo imeshacheza mpaka sasa.
Mtibwa ambayo ilishuka daraja msimu uliopita na sasa wamerejea rasmi huku ikiwa imeweka rekodi ya kucheza michezo 14 katika uwanja wao wa nyumbani wa Manungu pasipo kufungwa huku michezo 14 ya ugenini wakishinda saba kupata sare nne na kufungwa michezo mitatu.
Aidha timu hiyo imefanikiwa kufunga mabao 54 kuruhusu mabao 16 katika michezo timu hiyo iliyocheza huku wakiwa wamebaki na michezo miwili ili kuweza kutamatika kwa Ligi ya Championship ya NBC