LIGI Kuu ya NBC imeendelea kushika kasi ikiwa ni mzunguko wake wa tisa kwa timu ya Young Africans na Mashujaa, huku timu ya Young Africans ikiondoka na alama tatu muhimu za mchezo huo ulichezwa kakika uwanja wa KMC Complex saa 12:30 jioni, DSM, ambapo timu ya Young Africans ilikuwa mwenyeji wa timu ya Mashujaa.
Kipindi cha kwanza cha mchezo huo kilianza kwa kasi huku timu zote mbili zikionesha ushindani mkubwa ili kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri zaidi, lakini iliwachukua dakika saba kwa timu ya Mashujaa kufungua ukurasa wa mabao kupitia mchezaji wake Chrispin Ngushi.
Pia kwa upande wa timu ya Yanga walizidi kuonesha ubora wao kwa kumiliki mchezo kwa asilimia kubwa zaidi huku ikimchukua dakika 21 Peter Shalulile kufunga bao la kusawazisha hivyo timu hizo zikienda mapumziko 1-1.
Kipindi cha pili kilirejea huku timu zote mbili zikicheza kwa kujilinda zaidi ili kutoruhusu makosa yatakayopelekea kupoteza alama za mchezo huo, iliwachukua dakika 76 timu ya Young Africans kuongeza bao la ushindi kupitia mchezaji wake Clement Mzize na mchezo kutamatika kwa matokeo ya 2-1.
Clement Mzize wa timu ya Young Africans ndiye alichukua tuzo ya mchezaji bora wa mchezo huo kutokana na umahiri aliouonyesha katika mchezo huo.