POLISI, YOUNG AFRICANS WAMALIZA WIKI VEMA LIGI KUU YA NBC.

Polisi Tanzania imepata ushindi wa kwanza msimu huu kwenye uwanja wa Ushirika, Kilimanjaro dakika za mwisho baada ya kuifunga Geita Gold bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo ilibidi kusubiri hadi dakika za nyongeza Isaya Kuzoza wa Geita Gold kujifunga na kuipa Polisi Tanzania ushindi wa bao moja.

Ushindi huo unaifanya Polisi Tanzania kujikusanyia alama tatu muhimu na kuwa ushindi wa kwanza msimu huu kwenye uwanja wa ushirika kwa Maafande hao huku Geita Gold ikiondoka patupu.

Katika mchezo mwingine uliochezwa saa 1:00 usiku kwenye uwanja wa KMC Complex timu ya Yanga iliwakaribisha Kagera Sugar na ‘wananchi’ kuichapa Kagera Sugar mabao 4-0.

Mshambuliaji Peter Shalulile alianza kuandika ushindi wa Yanga dakika ya 26, kabla ya Mohamed Hussein kuongeza bao la pili dakika ya 32 na kuifanya timu hiyo kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili, Yanga iliendelea kutawala mchezo na kupata mabao mawili kupitia kwa Cheikh Toure aliyefunga dakika 83 na 90+7 akihitimisha ushindi wa mabao 4-0.

Matokeo haya yanaifanya Yanga kuondoka na alama tatu muhimu ikiishusha Azam nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 27.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *