FAINALI ya kombe la Mapinduzi inachezwa leo januari 13 kwenye uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar ambapo mwakilishi pekee wa Ligi Kuu ya NBC Simba itacheza dhidi ya Mlandege.
Hii ni mara ya 10 Simba kuingia fainali ya Kombe la Mapinduzi na kuandika historia kuwa timu iliyocheza fainali nyingi zaidi ya kombe hilo.
Mlandege inaingia kwenye fainali hii ikiwa kama bingwa mtetezi baada ya msimu uliopita kuifunga Singida FG kwenye fainali.