LIGI Kuu ya NBC inazidi kushika kasi ikiwa ni takribani michezo 183 imeshachezwa huku mabao 406 yakiwa yamefungwa ikiwemo yaliyofungwa kwa mguu wa kushoto na wakali wafuatao.
Ki Azizi ni kiungo mshambuliaji wa Young African katika msimu huu wa 2024/2025 ameshatia wavuni mabao sita kwa mguu wake wa kushoto kati ya mabao saba aliyofunga mpaka sasa.
Winga wa timu ya Azam, Gibril Sillah, ameshatia wavuni mabao matano kwa mguu wake wa kushoto kati ya saba ambayo ameshafunga mpaka sasa.
Offen Chikola wa Tabora United ameshatikisa nyavu mara tano kwa mguu wa kushoto kati ya mabao saba aliyofunga msimu huu.
Nassor Saaduni ni mshambuliaji wa Azam akiwa amefanikiwa kuingia langoni mwa wapinzani wao mara tano akitumia mguu wake wa kushoto.
Mchezaji Selemani Bwenzi aliyeingia dirisha dogo kwa timu ya KenGold mkali huyo mpaka sasa amefanikiwa kutikisa nyavu za wapinzani akitumia mguu wake wa kushoto.
Naye mchezaji wa Namungo Joshua Ibrahimu kafanikiwa kuweka mpira wavuni mara nne akitumia mguu wake wa kushoto.