HASHIKIKI hivyo ndivyo unavyoweza kusema kutokana na Kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba,Jean Ahoua, kutokana na mchezaji huyo kuwa na namba nzuri za mabao ndani ya Ligi Kuu ya NBC kwa msimu huu wa 2024/2025.
Ikiwa ni msimu wake wa kwanza ndani ya Simba akitokea nchini kwao Ivory Coast mchezaji huyo amefanikiwa kufunga mabao 12 kati ya mabao 52 ambayo timu ya Simba imefunga katika michezo 22 hadi sasa huku akifuatiwa na Clement Mzize mwenye mabao 10 sawa na Prince Dube ambao ni wachezaji Young African.
Ahoua amefunga mabao katika michezo ya Simba dhidi ya timu za Fountain Gate (1), Dodoma Jiji (1), Namungo (1), KMC (2), Kagera Sugar (1), JKT Tanzania (1), Tanzania Prisons (1), Namungo dhidi ya Simba (2) na Simba dhidi ya Dodoma Jiji (2).
Ahoua amekuwa na msimu mzuri kwenye Ligi Kuu ya NBC akishika nafasi ya tatu kwenye vinara wa pasi za mabao baada ya kutoa pasi saba hadi sasa.
Kanuni ya ligi kuu