LIGI Kuu ya NBC imeendelea jana ambapo mchezo wa Dabi ya Dar es Salaam ambapo Azam iliwakaribisha Young Africans uliochezwa katika uwanja wa Azam Complex majira ya saa moja usiku.
Mchezo huo ulianza kwa kasi kubwa huku Young Africans wakionekana kushambulia kwa kasi kubwa huku Azam wakionekana kuzuia kwa kasi ya wapinzani wao.
Ilimchukua dakika 11 tu kiungo wa Young Africans Pacome Zouzoua kufungua ukurasa wa mabao ambapo aliitanguliza timu yake huku Prince Dube akiongeza bao dakika ya 34 ya mchezo huo na kufanya timu hiyo kwenda mapumziko wakiwa wako mbele kwa mabao 0-2.
Kipindi cha pili mchezo uliendelea kwa timu zote kusaka mabao ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi na dakika ya 81 beki wa Azam Lusajo Mwaikenda alifungua ukurasa wa mabao kwa timu yake hivyo kufanya mchezo kuwa wa kasi ya kushambuliana zaidi ambapo dakika 90 zilitamatika kwa matokeo ya 1-2.
Mshambuliaji wa Young Africans Prince Dube alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo baada ya kuisaidia timu yake kupata ushindi.
Yanga lazima ashide