LIGI Kuu ya NBC imeendelea ambapo JKT Tanzania waliikaribisha Namungo uwanja wa Isamuhyo mchezo uliochezwa saa nane mchana na kumalizika kwa sare ya 2-2.
Mchezo ulianza kwa kasi ambapo Namungo walishambulia lango la JKT na dakika ya 18 Saleh Karabaka aliipatia timu yake bao la kwanza kabla ya dakika ya 49 Fabrice Ngoy kuongeza bao la pili.
Kipindi cha pili JKT Tanzania walirudi kwa kasi baada ya kutambua makosa yao na dakika ya 63 Maka Edward akaipatia JKT bao la kwanza na dakika ya 69 wakaongeza bao la pili lililofungwa na Shiza Kichuya.
Katika mchezo huo mchezaji bora alikuwa Shiza Kichuya wa JKT Tanzania aliyetengeneza bao la kwanza kwa mpira wa kona huku akifunga bao la kusawazisha kwa timu yake.
Kwa matokeo hayo JKT inafikisha alama 32 na kushika nafasi ya saba huku Namungo ikishika nafasi ya 11 baada ya kukusanya jumla ya alama 28.