BODI YA LIGI KUU TANZANIA (TPLB) KUPOKEA MAONI YA MABORESHO YA KANUNI ZA LIGI

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inaujulisha umma kuwa leo Julai 11, 2025 imeanza rasmi kupokea maoni ya maboresho ya Kanuni za Ligi kuelekea msimu wa 2025/2026.

Zoezi hilo la kupokea maoni litafanyika kwa kipindi cha majuma matatu ambapo litafungwarasmi Agosti 1, 2025.

Maoni ya maboresho ya kanuni yawasilishwe TPLB kwa kupitia njia zifuatazo;

i. Barua pepe – maoni@ligikuu.co.tz

ii. Ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) – +255 758 500 222

iii. Kuwasilisha kwa mkono katika ofisi za Bodi ya Ligi Kuu Tanzania zilizopo ghorofa

ya 14 kwenye jengo la NSSF (Mafao House), Ilala Dar es Salaam.

Bodi inawaomba wadau wote wa Ligi Kuu ya NBC, Ligi ya Championship ya NBC, First League na mpira wa miguu kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika zoezi hili muhimu kwa maendeleo ya Ligi zetu kwa kuchangia maoni yatakayosaidia kuboresha kanuni zake.

Wadau wanakumbushwa kuwa kanuni bora ndio msingi wa kupatikana kwa ligi bora na maendeleo ya mpira wa miguu kwa ujumla hivyo ushiriki katika zoezi hili ni jambo la muhimu sana.

15 comments

  1. 1: kanuni inayoruhusu mdhamini mmoja kudhamini timu zaidi ya mbili si rafiki kwenye ligi yetu kwasababu inatoa mwanya wa kupanga matokeo baina ya timu zinazodhaminiwa na mdhamini huyo.

    2: idadi ya wachezaji wa kigeni wanaoruhusiwa kujumuishwa kwenye mechi za ligi zetu zote ipunguzwe kwenye mechi za ligi kuu badala ya kuruhusu wachezaji wanane sasa ni vema ikibadilishwa na ikawa si zaidi ya wachezaji watano kwa mechi.

    1. Maoni yangu ni kwenye play off ingependeza timu za ligi kuu zikutane zenyewe anayefungwa ashuke na anayeshinda abaki na za championship anayeshinda apande ligi kuu na anayefungwa abaki championship na iwe mechi moja kwenye neutral ground

  2. 1 Kwanza kabisaa ni juu usajili wa chezaji wa mgeni idadi ni kubwa kitu kinachopelekea kupoteza kipaji vya wazawa leo hii club kama singda black stars first eleven unamkuta mzawa mmoja tu matokeo yake aina mchezaji yeyote timu ya taifa sas wanachango gan katika taifa
    2 kama biashara united alikatwa 15 point kisa kukosa michezo je nn kinaleta ukakasi katika vilabu vyetu vya kariakoo sharia update mkondo wake akuna cha timu ya mwigulu wala majaliwa kanuni isimamiwe na kupitia hivi atutaona watu wakizionea timu ndogo kisa tu wanajiweza kiuchumi
    3 GSM plus GIBOOST hiii sio sawa mzamini mmoja inawezekanaje azizamin timu 8 hiii sio sawa ata kidogo ndo maana USHINDANI akuna bingwa wa ligi kazi yake kuishia makundi na yule ambae ata sio bingwa iones shughuli yake sio ya katoto ebu kuweni serious kidogo

  3. Sheria ya timu za ligi kuu na championship kucheza play off ibadirishwe timu za ligi kuu ziporomoke moja kwa moja na championship zipigane wenyewe kwa wenyewe anayeshinda apande
    Viongozi wawajibike kwa madudu yao yanapotokea sio kitiliana huruma na busara .
    Klabu kimoja kudhaminiwa na kampuni moja sio kampuni moja timu zaidi ya moja

    1. Maoni yangu ni kwenye play off ingependeza timu za ligi kuu zikutane zenyewe anayefungwa ashuke na anayeshinda abaki na za championship anayeshinda apande ligi kuu na anayefungwa abaki championship na iwe mechi moja kwenye neutral ground

  4. Habari, naitwa JOVINUS Naishi Temeke, kwanza ninawashukulu kwa kutupa nafasi ya kutowa maoni yetu, ila ninaomba muyazingatie, 1). Ninapendekeza katika ligi kuu NBC kuna makosa timu zinafanya zinapimwa fani ya kulipa ela nigeshauli timu ikionekana inafanfa vitu vyenye kuashilia ushilikina, kupitia mlango usio lasmi, Gari kuingia kinyume nyume, timu inyanganywe point 3 na faini juu, vitendo hivyo vitaisha.

    2). NBC Champions ship, timu zinazocheza playoff Timu itakayo shida ipande ligi kuu moja kwa moja isicheze tena playoff.
    Vile vile NBC Premier league Timu itakayo shida ibaki ligi kuu, na itakayo fungwa nishuke moja kwa moja bila ya kucheza na timu ya Champions ship, ASANTE.

    1. Habari za leo waheshimiwa.
      Maoni yangu kwa kanuni za ligi kuu tz, ni kwa waamuzi endapo waamuzi wameshindwa kusimamia kanuni isiishie kupewa adhabu pekee na matokeo yatenguliwe. Kwa mfano timu zilikua droo halafu kanuni ikavunjwa timu moja ikanufaika basi yatenguliwe matokeo ya mnufaikaji baada ya kujiridhisha na mwamuzi kupewa adhabu anayostahili. Kwa sababu timu nyingi zinajitahidi kusajili kwa gharama kubwa wachezaji kisha wanahujumiwa na waamuzi na istoshe mwamuzi anapewa adhabu na bado matokeo yako pale pale kitu ambacho hakinufaishi timu iliyodhulumiwa na wala timu iliyonufaika na maamuzi mabaya ya muamuzi aliyeadhibiwa yapo vile vile hayajamuathiri kwa chochote. Ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia maoni yangu. Naitwa Shabani Ndonghwe wa Kilimanjaro.

  5. Kungekua na kanun ambazo nitafanya matokeo yawe yanapatikana kwa haki mfano refa anaponufaisha timu moja huku tunajionea kabsa na huyo refa kufungiwa na hyo timu kupata point 3 szan kma inasaidia kitu kma kuna uwezekano wa kupokwa point ufanyike kwenye matukio ambayo yako Open sana maana inafanya kupoteza Radha nzim ya mchezo.

    2.kanuni ziwe Kali kwa refaree wote ambao wataonekana kuwa wamechezesha mchezo kinyume na sheria.

    3.mda wa nyongeza katika mchezo usiangalie masilahi ya timu furani Bali ukae kimkakati ambapo utasaidia mchezo kuchezek kwa dakika 90 haijalishi mkubwa au mdogo kapoteza.

    4.pongezi kwa azam media yote kwa ujumla kwa mmbo ambayo wanayafanya kwenye soka letu hapa Tanzania na afrika kwa ujumla. Pia ningependa waweze kuboresha zaidi na zaidi.

  6. NAOMBA KUTOA MAONIYANGU KTK VIPENGELE VYA:-
    1. FAINI ZA MAKOSA MBALIMBALI;
    A. KADI 3 ZA NJANO; MCHEZAJI ALIPE FAINI 500,000/= NA KUKOSA MICHEZO MIWILI.
    B. STRAIGHT RED CARD; MCHEZAJI ALIPE FAINI 1,000,000/= NA KUKOSA MICHEZO MIWILI.
    C. TIMU KUPEWA KADI ZA NJANO ZAIDI YA TANO KWENYE MICHEZO MMOJA: FAINI 5,000,000/=
    2. UDHAMINI WA TIMU SHIRIKI ZA LIGI KUU;
    KILA TIMU IWE NA MDHAMINI WAKE AMBAYE SI AZAM AU NBC AMBAO WATAZIWEZESHA KIUCHUMI TIMU ZOTE.
    PIA, NI LAZIMA KILA TIMU KUWEPO NA TIMU
    U.15
    U-17,
    U-20
    KTK MAKUNDI YOTE WANAWAKE NA WAVULANA.
    3. KILA TIMU IWE NA UWANJA WAKE RASMI WA MAZOEZI.
    4. WAMILIKI WA VIWANJA WAFANYE UKARABATI WA KURIDHISHA ILI KUEPUKA TIMU MGENI KUINGIZA GHARAMA KWA KUHAMIA TIMU KUTOKA MKOA MMOJA KWENDA MKOA MWINGINE.
    SIGN OFF.
    MABULA ENOX BABAAH,,,

  7. Udhaminu wa mtu anaefadhili club moja alio na maslahi nayo hawez kuruhusiwa kudhamini club zingine za liguu ilikuondoa mgongano wa ki maslai bain ya vilabu hivyo
    Vilabu kuchunguzwa utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu kabla ya mechi na wakati wa mapumzigo

  8. Naitwa AIDAN MBINGA kutoka TUNDUMA – SONGWE

    MAONI YANGU
    1. Swala la mdhamini mmoja kudhamini zaidi ya timu Moja ni kiashiria Cha wazi Cha upangaji wa matokeo. Hata kama ni Kwa ajili ya afya ya vilabu vyetu hili swala liangaliwe upya.

    2. Kwenye play offs napendekeza vilabu vya logo KUU vicheze vyenyew na championship vicheze vyenyew. Anayeshinda abaki, anayefungwa ashuke

    3. Adhabu Kwa timu zinazokiuka kanuni Kv. Kuvunja geti, kupitia milango isiyo rasmi na viashiria vingine vya ushirikina iwe kubwa zaidi kuanzia Milioni 50 na timu ikirudia iwe kukatwa point 3 siyo faini ya fedha tena. Hivi vilabu vikubwa vinaona vina uwezo kifedha na nguvu ya kuchangisha Kwa mashabiki hivyo vinavunja kanuni makusudi.

    4. Kanuni zitumike Kwa usawa Kwa timu zote za LIGI KUU, kitendo Cha timu Moja kugomea mchezo bila sababu na kuachwa huku timu nyingine ikigomea inaadhibiwa kinaiweka LIGI yetu kwenye hatari ya kupoteza hadhi na thamani yake hivyo kuweka hatarini msitakabali wake.
    (Matumizi ya busara badala ya kanuni hakileti afya kwenye mpira wetu)

    5. Kanuni inayounda bodi ya ligi kuu iwe huru, viongozi wachaguliwe Kwa uhuru na timu zote za LIGI KUU na iwekwe akidi ya asilimia ngapi ya vilabu vikipiga kura ya kumtaka kiongozi ajiuzulu basi atafanya hivyo. Tusiruhusu siasa ziingilie mpira ni hatari Kwa mpira wetu.

    ASANTE

  9. 1. Napendekeza UDHAMINI wa kampuni, TAASISI kwa club uwe ni kampuni moja kwa club MOJA tu,nyongeza ni kama kampuni inabranch za makampuni tanzu nayo yasiruhusiwe kabisa kudhamini club nyingine mfano AZAM na bakhresa group of companies wasiruhisiwe KUTOA msaada au udhamini kwa club nyingine

    2. SIASA iwekewe kipengele maalum ipigwe marufuku kikanuni kuwa wanasiasa ni marufuku kutumia influence zao za kisiasa kuingilia SOKA kwa MASLAHI ya vilabu,mwisho iwe ushangiliaji Tu na POROJO za kawaida

    3.Isiruhusiwe KIONGOZI wa club MOJA kuongoza club nyingine kwa namna yeyote ile mfano MO DEWJ ni RAISI WA HESHIMA wa SIMBA na mdhamini hatakiwi kujihusisha kabisa na SINGIDA au NAMUNGO kwa namna yeyote hata msaada Gizani ikibainika kifungo MAISHA,au MWIGULU nchemba,w)MAVUNDE (W),majaliwa kassim(pm) wao wanaintrest na vilabu vingine na ni viongozi wa Dodoma, SINGIDA na NAMUNGO wasiruhisiwe kuongoza Simba,au YANGA au kutoa misaada ya wazi/kizani ikibainika wafungiwe MAISHA

    4. Kusiwepo na double standard ya ADHABU pamoja na upana wa kanuni za LIGI adhabu itakayotolewa na TPBLB kwa club iwe ni mfano wa kesi za MAHAKAMA,kwamba kwa kosa hilohilo club MOJA inaonywa na nyingine inapigwa fine,mfano msimu uliopita YANGA amefanya vitendo vya KISHIRIKINA zaidi ya mara MOJA kwa kujirudia rudia wamegoma kupitia mageti yanayotakiwa mara kadhaa lkn adhabu ni maonyo na wengine kutochukuliwa HATUA kabisa kwa matendo ya KISHIRIKINA ambayo yameonekana waziwazi na kama ni fine zinakuwa nyepesi ,ikibainika kuna UPENDELEO viongozi waliohusika kufanya upendeleo huo watozwe fine isiyopunguan10,000,0000/= ili kuweka NIDHAMU

    5. Ufungiwaji wa waamuzi usiwe wa kuigiza kama inavyofanyika sasa ,ambapo anafungiwa REFA mechi kumi au MAISHA kwa huipendelea SIMBA/YANGA lkn siku ya mechi za mmoja Kati Yao anarejeshwa ili kuchezesha mechi hizohizo na anampendelea yuleyule kisha anaadhibiwa tena kukomesha hili DERBY za SIMBA na yanga waamuzi watoke NJE Ya Tanzania kwa gharama za timu mwenyeji(wanakatwa kwenye gate collection)tena wawe wenye weledi sio kama wa game ya BERKANE
    NA SIMBA

    6. Marefa wanaofungiwa wakirudi waende Kwanza CHAMPIONSHIP na wapewe mafunzo maalum wakati wanaangaliwa miendendo Yao kabla ya kurejea NBC PREMIER

    7. TPLB(BODI YA LIGI TANZANIA) isiruhusu jambo la BODI kuongelewa na mjumbe KATIBU au mwenyekiti na akifanya hivyo anakuwa amepoteza nafasi yake mojakwamoja MSEMAJI awe ni afisa HABARI wa bodi baada ya vikao maalum,hii itaondoa kabisa dhana ya viongozi wa bodi kuviwakilisha vilabu hasa Simba na YANGA baadala ya BODI ya LIGI ,ikumbukwe hawa ni binadamu na hapana shaka wanamapenzi na vilabu VYAO hivyo lazima watataka visogee mbele

    8. Wadhamini wakuu au wenza mfano NBC,CRDB,NMB, N.K viongozi wao iwe marufuku kujinasibu vilabu wanavyopenda mfano ni wazi NSEKELA ambaye ni CEO wa CRDB na mdhamini mkuu wa KIKOMBE CHA FEDERATION amewahi kujinasibu mapenzi kwa YANGA ikitokea hivyo watozwe fine ya 30,0000,0000/= na akirudia iwe 100,000,000/= kisha kifungo cha MAISHA kwa kujirudia mara ya 3

    9. Kanuni zimtake RAISI WA JAMUHURI,JAJI MKUU,WAZIRI MKUU,SPIKA,MAKAMU WA RAISI,WAKUU WOTE WA VYOMBO WAKIWA MADARAKANI kuwa NEUTRAL KIVITENDO(MICHANGO kifedha za SERIKALI) au maamuzi hii itauimarisha MPIRA na kuongeza NIDHAMU ya mpira bila kuichonganisha SERIKALI na watu wake

    ///// Utekelezaji mwema///////

  10. Katika kanuni za msimu huu kuwe na kanuni inayowahusu wachambuzi na sifa wanazopaswa kuwa nazo,nashauri kanuni iweke kigezo cha angalau mchambuzi wa michezo awe na leseni ya caf C,Ili awe na sifa ya kuajiliwa kama mchambuzi wa michezo kwa sababu itasaidia kujenga uwezo wa watu wengi kuuelewa Mpira wa miguu kwa faida ya kizazi Cha Sasa na kijacho. Wachambuzi wengi waliopo sasa wanapotosha sana jamii kwa sababu wengi wao hawauelewi kwa upana mpira wa miguu ndio maana wengi wanatumia muda mwingi kujadili mambo yasio na tija kwenye.Pia nashauri mdhamini mmoja asidhamini zaidi ya club Moja ili kuondoa uwezekano wa upangaji wa matokeo. Mwisho nashauri kwennye kanuni kuongeza idadi ya wachezaji wa kigeni kufikia 15 ili kuongeza chachu ya ushindani kwa wachezaji wetu wa ndani.

Join the Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *