MICHEZO miwili ya Ligi Kuu ya NBC itaendelea leo, Juni 16 huku timu zikisaka alama muhimu katika hatua za mwisho wa msimu kuhakikisha zinafikia malengo yao ya msimu huu.
Mchezo wa mapema utawakutanisha Namungo na TRA United kwenye Uwanja wa Majaliwa, mkoani Lindi kuanzia saa 10:00 alasiri, Namungo ikiingia kwenye mchezo huo ikiwa katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi na alama 26 huku TRA United ikishika nafasi ya 6 na alama 40 jambo linaloifanya mechi hiyo kuwa ya ushindani mkubwa.
Azam itakuwa mwenyeji wa Mashujaa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, mchezo utakaoanza saa 1:00 usiku.
Azam inashika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi na alama 55 ikisaka kuimarisha nafasi yake katika mbio za juu, huku Mashujaa wakiwa nafasi ya 11 na alama 27, wakipambana kuongeza alama muhimu zitakazowaweka salama kwenye msimamo.
Mashabiki wanatarajiwa kushuhudia michezo yenye ushindani mkubwa huku kila timu ikipigania kutimiza malengo yake kabla ya msimu kumalizika.