HAKUNA MBABE RUANGWA, AZAM IKIJIIMARISHA LIGI KUU YA NBC.

 

 

Namungo na TRA United zimeshindwa kutambiana nguvu baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa leo majira ya saa 10: 00 alasiri uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi.

 

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa uliwashuhudia pande zote zikitengeneza nafasi kadhaa za kufunga, lakini uimara wa safu za ulinzi pamoja na walinda milango ulihakikisha hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake hadi dakika 90 zinakamilika. 

 

Matokeo hayo yanaifanya kila timu kujiongezea alama moja muhimu katika hatua za mwisho za msimu huku TRA United ikiendelea kubaki ndani ya nafasi za juu zaidi kuliko Namungo kwenye msimamo wa ligi. 

 

Jofrey luzendaze wa TRA United alitajwa kuwa mchezaji bora wa mechi kutokana na mchango wake kwa timu kupata alama tatu.

 

Katika mchezo mwingine Azam imeendelea kuonyesha ubora wake katika mbio za kumaliza msimu wa Ligi Kuu ya NBC kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mashujaa katika mchezo uliochezwa leo saa 1:00 jioni kwenye uwanja wa Azam complex chamazi.

 

Mabao ya Azam yalifungwa na Sadio Kanoute dakika ya 39 kabla ya James Akaminko kuongeza la pili dakika ya 41 na kuwapa Wanalambalamba ushindi muhimu. 

 

Mchezaji Bora wa Mchezo James Akaminko ndie aliyeng’ara zaidi baada ya kufunga bao la kwanza na kuwa na mchango mkubwa katika ushindi wa timu ya Azam.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *