YOUNG AFRICANS,SIMBA ZATAMBA MZUNGUKO 28 LIGI KUU YA NBC.

MZUNGUKO wa 28 wa Ligi Kuu ya NBC umetamatika ambapo mechi zote nane zimechezwa majira ya saa kumi jioni huku ikisalia mizunguko miwili Ligi hiyo kutamatika.

Young Africans ilikuwa mwenyeji wa timu ya Azam katika uwanja wa Amaan Zanzibar ambapo iliishushia kipigo cha mabao 3-0 yalifungwa na Ibrahim Hamad, Laurindo Dilson na Pacome Zouzoua hivyo timu hiyo kujikita kileleni.

Mtibwa Sugar ilikuwa mwenyeji wa timu ya Simba katika uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo timu hiyo ilipoteza mchezo huo kwa 0-3 mabao ya Simba yakifungwa na Rushine De Reuck, Seleman Mwalimu na Anicet Aura.

Pamba Jiji iliialika timu ya Mbeya City katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo timu hiyo ilijikuta ikipokea kichapo cha 0-2 kwa mabao yaliyofungwa na nahodha wa Mbeya City Eliud Ambokile.

KMC ilicheza na Namungo ambapo ilikubali kichapo cha 2-3 huku mabao ya KMC yakifungwa na Erick Mwijage pamoja na Mohamed Abdallah huku mchezaji wa Namungo, Fabrice Ngoy akifunga yote matatu yaani (hat-trick).

Singida Black Stars ilicheza na Tanzania Prisons katika uwanja wa Airtel Singida ambapo timu hiyo iliibuka na ushindi wa 3-1 huku mabao ya Singida yakifungwa na Mossi Nduwumwe (2) na Kennedy Juma huku Kelvin Sangati akiifungia Prisons bao moja.

Fountain Gate ilikubali kichapo cha 0-1 kutoka kwa timu ya Mashujaa katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Black Rhino, Karatu Arusha na bao la Mashujaa likifungwa na Hussein Juma.

TRA ilikuwa mwenyeji wa timu ya Coastal Union katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha ambapo mpaka mchezo unatamatika matokeo yalikuwa sare ya 1-1, bao la TRA lilfungwa na Nasri Kombo huku Maabad Maabad akiifungia Coastal bao la kusawazisha.

Mchezo wa mwisho ulikuwa Dodoma Jiji dhidi ya JKT Tanzania katika uwanja wa Jamhuri Dodoma ambapo mchezo huo ulitamatika kwa matokeo ya 0-0.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *