MOSSI, FEISAL HAPATOSHI VITA YA UFUNGAJI BORA

VITA ya ufungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC imeanza upya baada ya mshambuliaji wa Singida Black Stars Mossi Ndumumwe kufikia idadi ya mabao aliyokuwa nayo kiungo wa Azam,Feisal Salum.

Mossi Ndumumwe anaekipiga kunako Singida Black Stars amecheza michezo 20 sawa na dakika 1622 huku akifanikiwa kuingia nyavuni mara 14 pasipo kuwa na bao lolote la mkwaju wa penati.

Feisal Salum wa Azam amefanikiwa kucheza michezo 26 ya Ligi Kuu ya NBC sawa na dakika 2095 huku akiingia nyavuni mwa wapinzani wake mara 14.

Methew Tegisi wa Pamba Jiji ameshacheza michezo 22 sawa na dakika 1567 amefanikiwa kutikisa nyavu mara 11.

Allan Okello wa Young Africans amecheza michezo 22 ya Ligi Kuu ya NBC mpaka sasa sawa na dakika 1567 huku akitikisa nyavu za wapinzani mara 11.

Fabrice Ngoy wa Namungo amecheza michezo 27 sawa na dakika 1720 ambapo amefanikiwa kufunga mabao 11.

Mudathir Yahya wa Young Africans nae hayuko mbali amecheza michezo 20 sawa na dakika 1253 na kufanikiwa kufunga mabao tisa.

Pacome Zouzoua wa Young Africans ameshacheza michezo 20 ya Ligi Kuu ya NBC sawa na dakika 1422 amefanikiwa kufunga mabao tisa.

Selemani Mwalimu wa Simba amecheza michezo 23 sawa na dakika 1102 amefanikiwa kuingia golini mara tisa huku.

Prince Dube wa Young Africans amefanikiwa kucheza michezo 24 ya Ligi Kuu ya NBC sawa na dakika 1742 na kufunga mabao tisa.

Start a Conversation

Your email address will not be published. Required fields are marked *