MCHAKAMCHAKA wa Ligi Kuu ya NBC unaendelea tena leo kwa michezo miwili ya ‘kibingwa’ kwenye mikoa miwili tofauti.
Saa 10:00 alasiri KMC wataialika Simba katika uwanja wa Azam Complex mkoani Dar es salaam.
KMC itatumia uwanja wa Azam Complex kama uwanja wao wa Nyumbani baada ya uwanja wa Uhuru kuwa katika marekebisho.
Tabora United watakuwa wenyeji wa Yanga katika uwanja Jamhuri mkoani Dodoma saa 1:00 usiku.
Tabora United wanatumia uwanja wa Jamhuri, Dodoma kama uwanja wao wa nyumbani badala ya Ali Hassani Mwinyi licha ya kufunguliwa, hii ni kwasababu uwanja huo upo katika uangalizi wa siku saba tangu ulipofunguliwa Desemba 21, kama kanuni ya Ligi Kuu toleo la 2023 inavyoelekeza.