LADHA ya Ligi Kuu ya NBC iliendelea leo kwa michezo mitatu iliyochezwa kwenye viwanja vitatu tofauti.
Saa 8:00 mchana Tanzania Prisons walikua wenyeji wa Namungo katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Tanzania Prisons kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Samson Mbangula dakika ya 42 ya mchezo.
Saa 10:00 jioni Geita Gold waliwaalika Singida FG katika uwanja wa Nyankumbu na Geita kuibuka na ushindi wa bao 1 likifungwa na Mchezaji Valentino Mashaka Kusengama dakika ya 79 ya mchezo.
Mchezo wa mwisho ulizikutanisha Kagera Sugar dhidi ya Azam katika uwanja wa Kaitaba Mkoani kagera na kumalizika kwa Kagera Sugar kukubali kichapo cha mabao 4-0.
Kwa matokeo haya Azam anazidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC akifikisha jumla ya alama 31 huku akiwa amecheza michezo 13 tofauti ya alama nne na Yanga anayeshika nafasi ya pili huku akiwa amecheza michezo 10 .