Author: Loveness Bernard

SINGIDA YAONGEZA MAUMIVU KWA MTIBWA.

SINGIDA Black Stars imejipata baada ya kuifunga timu ya Mtibwa Sugar mabao 3-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa leo katika uwanja wa Jamhuri Dodoma majira ya saa nane mchana.

Iliwachukua dakika tano pekee Singida kufungua ukurasa wa mabao kupitia mchezaji wao Nduhumwe Mosi na dakika ya 16 Horso Muaku aliiongezea timu hiyo bao la pili hivyo kwenda mapumziko wakiongoza kwa mabao mawili.

Wachezaji wa Singida wakishangilia bao.

Kipindi ca pili timu zote zilikuwa na ari ya kutaka ushindi hasa Mtibwa iliyokuwa nyuma kwa mabao mawili hata hivyo ndoto zao zilizidi kudidimia baada ya Kennedy Juma kuongeza bao la tatu kwa timu ya Singida ikiwa ni dakika ya 58 ya mchezo huo.

Dakika ya 88 Mtibwa ilipata bao la kufutia machozi kupitia mchezaji wao Raizin Haji hivyo kufanya mchezo kumalizika wa 1-3 na Singida kufanikiwa kubeba alama zote tatu ugenini huku mchezaji wa Singida Horso Muaku alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.

DODOMA JIJI WAJIPATA JAMHURI

Timu ya Dodoma Jiji imejipata katika uwanja wake wa nyumbani wa Jamhuri baada ya kuhakikisha wanashinda kila mchezo wawapo hapo.

Dodoma ambayo imecheza na timu ya TRA United jana imefanikiwa kushinda michezo minne katika uwanja huo,sare mbili na huku ikipoteza mchezo mmoja tu katika michezo saba ambayo timu hiyo imecheza uwanjani hapo.

Mchezaji wa Dodoma Jiji,Dickson Mhilu

Katika mchezo wa jana ulionza majira ya saa moja usiku Dodoma ilionekana ikizitaka alama zote tatu kutoka kwa TRA kwani timu hiyo ilitawala mchezo ambapo dakika ya 15 ya mchezo huo Faraji Kayanda alifungua ukurasa wa mabao.

TRA nayo ilionekana ikiuta ka mchezo kwa kutaka kusawazisha hata hivyo ndoto yao ilizimwa na mchezaji wa Gadiel Michael ambaye aliongeza bao la pili kwa timu yake hivto kwenda mapumziko Dodoma ikiwa mbele kwa mabao mawili.

Kipindi cha pili kilirejea ambapo dakika ya 55 Edgar William alizidi kudidimiza matumaini ya TRA baada ya kuongeza bao la tatu kwa timu yake ambapo mpaka mchezo unatamatika Dodoma iliibuka na ushindi wa 3-0 hivyo timu hiyo ilipanda kutoka nafasi ya saba hadi ya sdita katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.
[13/02/2026, 09:26:53] Honest Tplb: mkuu

LIGI KUU YA NBC ‘KUCHANJA MBUGA’ LEO.

LIGI Kuu ya NBC itaendelea leo kwa michezo miwili itakayochezwa katika mikoa ya Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba na Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine.

Mchezo wa kwanza utakuwa saa 8:00 mchana ambapo timu ya Pamba Jiji ya Mwanza itaialika timu ya Coastal Union ya Tanga katika ‘dimba’ la Kirumba.

Pamba Jiji inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikicheza michezo 12 ikishinda minne, sare tano na kufungwa mitatu huku ikikusanya alama 17.

Coastal ipo nafasi ya 12 katika msimamo ikicheza michezo 12 ikishinda miwili, sare tano na kufungwa michezo mitano huku ikikusanya alama 11.

Mchezo wa pili leo utakuwa majira ya saa 10:15 alasiri ambapo timu ya Tanzania Prisons itaialika timu ya Mashujaa katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.

Prisons ipo nafasi ya 15 ikiwa imekusanya jumla ya alama nane ikiwa imeshinda michezo miwili, sare mbili na kufungwa michezo sita.

VIWANJA VIWILI KUWAKA MOTO LIGI KUU YA NBC LEO.

LIGI Kuu ya NBC leo itaendelea mkoani Dar es Salaam katika viwanja viwili ambapo timu ya Simba itakuwa mwenyeji wa Mashujaa katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo majira ya saa 10:00 alasiri huku timu ya Azam ikiwaalika TRA katika uwanja wa Azam Complex Chamazi saa 1:00 usiku.

Simba ipo nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa imecheza michezo sita, ikishinda michezo minne, sare moja na kufungwa mchezo mmoja huku ikikusanya alama 13.

Mchezaji wa Azam, Zidane Sereri

Mashujaa ipo nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikicheza michezo 10, ikishinda michezo mitatu, sare nne na kufungwa michezo mitatu huku ikikusanya alama 13.

Kwa upande wa timu ya Azam imecheza michezo saba hadi sasa bila kupoteza ikishinda michezo mitatu na sare nne na kufanikiwa kukusanya alama 13 katika michezo hiyo.

Timu ya TRA United ipo nafasi ya tisa katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa imecheza michezo nane, ikishinda michezo mitatu, sare tatu na kufungwa michezo miwili huku ikikusanya alama 12.

DUKE,PEDRO WANG’ARA TUZO ZA DISEMBA

MCHEZAJI Duke Abuya wa Klabu ya Young Africans, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Disemba wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2025/26, huku Pedro Goncalves pia wa Young Africans akichaguliwa kuwa Kocha Bora wa Ligi hiyo kwa mwezi huo.

Duke alionesha kiwango kizuri chenye mwendelezo akiisaidia timu yake kushinda michezo miwili iliyocheza mwezi huo, pamoja na kuhusika katika mabao mawili kwa dakika 180 za michezo hiyo.

Mchezaji huyo aliwashinda Nassor Saadun wa Azam na Prince Dube wa Young Africans alioingia nao fainali katika mchakato wa Tuzo za Mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kwa upande wa Pedro aliyeingia fainali katika mchakato huo na Florent Ibenge wa Azam na Etienne Ndairagije wa TRA United, aliiongoza timu yake kushinda michezo miwili na kupaa kutoka nafasi ya nne hadi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo. Young Africans ilizifunga Fountain Gate (2-0), na Coastal Union (0-1).

Wakati huohuo Meneja wa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Said Mpuche, amechaguliwa kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Disemba kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

Mchezaji wa Transit Camp Adam Uledi

Katika hatua nyingine mchezaji wa Transit Camp, Adam Uledi, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Disemba wa Ligi ya Championship ya NBC 2025/26, huku Shadrack Nsajigwa pia wa Transit Camp akichaguliwa Kocha Bora wa mwezi huo.

Uledi aliyeingia fainali katika mchakato huo na Obrey Chirwa wa Kagera Sugar na Boniface Mwanjonde wa Mbeya Kwanza, alionesha kiwango chenye mwendelezo ikiwa ni pamoja na kucheza dakika 450 za michezo mitano aliyocheza.

Kwa upande wa Nsajigwa aliyeingia fainali na Juma Kaseja wa Kagera Sugar na Zuberi Katwila wa Geita Gold aliiwezesha timu yake kushinda michezo yote mitano iliyocheza mwezi huo.