LIGI ya NBC Championship mzunguko wa 17 inaanza leo kwa michezo miwili kupigwa kwenye mikoa miwili.
Mapema saa 8:00 mchana Cosmopolitan itakuwa mwenyeji wa Copco kwenye uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.
Cosmopolitan ipo nafasi ya 14 katika msimamo wa NBC championship baada ya kukusanya alama 14 katika michezo 16 huku Copco ikiwa nafasi ya 15 na alama 12 katika michezo 16.
Mchezo wa mwisho leo utazikutanisha Biashara United dhidi ya TMA kwenye uwanja wa Karume, Mara saa 10:00 alasiri.
Mchezo huu unabeba hisia za watu wengi kutokana na timu itakayoshinda itapanda hadi nafasi ya kwanza kwenye msimamo Biashara ikishika nafasi ya tatu na alama 33 kwenye michezo 16 sawa na TMA huku timu hizo zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.