MCHEZO wa kwanza wa mchujo wa timu za NBC Championship kupanda Ligi Kuu ya NBC Kati ya BIashara United na Mbeya kwanza umemalizika kwa Biashara United kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya kwanza.
Mabao ya Biashara United yamefungwa na Abeid Othman dakika ya 22 na Boban Bogere dakika ya 34 na Kuifanya Biashara United kuondoka na ushindi huo muhimu kwenye uwanja wake wa nyumbani.
Mchezo wa pili wa mtoano utachezwa Mei 26 saa 10:00 alasiri katika uwanja wa Nangwanda sijaona mkoani Mtwara ukiwa uwanja wa nyumbani wa Mbeya kwanza.
Mshindi wa jumla wa michezo hii atacheza na timu iliyofungwa kwenye mchezo utakaozikutanisha timu zilizoshika nafasi ya 13 na 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC na mshindi wa mchezo huo kushiriki Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025.