LIGI Kuu ya NBC imeendelea leo mkoani Tabora kwa mchezo uliozikutanisha timu ya Tabora United dhidi ya timu ya Namungo katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Mchezo huo uliochezwa majira ya saa nane mchana ulianza kwa kasi tangu mwanzo kwani dakika ya nne ya mchezo huo mchezaji wa Namungo, Jacob Massawe aliweka mpira wavuni mwa Tabora United.
Offen Chikola ndio alirejesha matumaini ya Tabora United katika dakika ya 32 ya mchezo huo ambapo alifunga bao na hivyo kuifanya mechi kwenda mapumziko wakiwa sare ya 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo dakika ya 52 mshambuliaji wa Tabora Heritier Makambo aliiongezea bao la pili timu yake na kufanya ubao kusomeka 2-1 pasi ya mwisho ikiwa imetolewa na Offen Chikola.
Mchezo ulitamatika kwa timu ya Tabora kubeba alama zote tatu mhimu za mchezo huo na mchezaji wao Offen Chikola akitangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.