Mzunguko wa tatu wa First league kundi B umetamatika kwa michezo minne huku Kigoma FC ikiendelea kuwa moto wa kuotea mbali.
Kigoma imeendelea kushika usukani wa msimamo ikiwa imecheza michezo mitatu akiwa na alama tisa na akifunga mabao nane na kuruhusu bao moja, timu hiyo kutoka mkoani Kigoma imeshinda michezo yote hadi sasa.
Madini United inafuatia katika nafasi ya pili ikiwa na alama sita baada ya kushinda michezo miwili na kupotesa mmoja, imekuwa na safu bora ya ushambuliaji iliyofunga mabao tisa huku ikiruhusu mabao matano.
Nafasi ya tatu inashikiliwa na Alliance yenye alama sita ikiwa imeshinda michezo miwili na kupoteza mmoja katika michezo mitatu, imefunga mabao sita na kuruhusu manne.
NKIM ya Tanga imekusanya alama sita na kushika nafasi ya nne baada ya kupata ushindi mara mbili na kupoteza mchezo mmoja ikiwa na mabao manne na ikifungwa mabao manne.
Endument ya Kilimanjaro inashika nafasi ya tano ikiwa na alama nne baada ya kushinda mchezo mmoja, kutoka sare ya bao moja na kupoteza mmoja, timu hiyo imefunga mabao matatu huku nyavu zake zikitikiswa mara nne.
Mt Hanang ya Manyara ipo nafasi ya sita katika msimamo wa kundi B ikiwa imecheza michezo mitatu, ushindi mchezo mmoja, na kufungwa michezo miwili huku ikifunga mabao manne na kuruhusu mabao sita, ikikusanya alama tatu.
Nafasi ya saba ipo timu ya Copco ya Mwanza ikiwa imecheza michezo mitatu, sare moja na kufungwa michezo miwili, aidha imefunga mabao manne na kuruhusu mabao tisa huku ikikusanya alama moja.
African Sports ya Tanga inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa kundi B ikiwa imecheza michezo mitatu na kufungwa michezo yote huku ikifunga mabao manne na kuruhusu mabao tisa ikiwa haina alama yoyote.