LIGI Kuu ya NBC imeendelea jana mkoani Manyara ambapo timu ya Fountain Gate Iliwakaribisha timu ya Simba katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa majira ya saa kumi alasiri.
Mchezo huo ulianza kwa kasi ambapo timu zote zilionekana kushambuliana kwa kasi kubwa huku kila timu ikionyesha nia ya kuzitaka alama tatu muhimu za mchezo huo jambo lilipolekea kwenda mapumziko wakiwa hawajafungana .
Kipindi cha pili kilianza ambapo dakika ya 57 mshambuliaji wa Simba, Leonel Ateba alifunga bao la kwanza kwa timu yake hivyo Simba kuwa mbele kwa 0-1.
Dakika ya 74 winga wa Simba Ladack Chasambi alijifunga goli baada ya kupiga mpira nyuma na golikipa wa Simba Moussa Camara kushindwa kuumudu ukaingia nyavuni hivyo ubao kusomeka 1-1 mpaka mchezo huo unatamatika.
Simba ilifanikiwa kuvuna alama moja ugenini na kufikisha alama 44 wakiwa nafasi ya pili ya msimamo wakiwa wamefunga mabao 35 na kufungwa 6 katika mechi 17 ilizocheza mpaka sasa.
 
					