TIMU ya Tanzania Prisons imerejea vema kwenye Ligi Kuu ya NBC baada ya kuifunga Mashujaa mabao 2-1 kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Mabao ya Prisons yalifungwa na Beno Ngassa mdogo wa nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania Mrisho Ngassa na Meshack Mwamita aliyefunga bao la ushindi kipindi cha pili huku bao la kufutia machozi kwa mashujaa likifungwa Seif Karihe kwa mkwaju wa penati.
Ukiwa mchezo wa kwanza kwa kocha mpya wa Prisons Amani Josiah kwenye Ligi Kuu ya NBC Prisons imesalia nafasi ya 13 ikifikisha alama 17 sawa na Namungo huku Prisons ikizidiwa kwa mabao ya kufunga.
Matokeo hayo yanaifanya timu ya Mashujaa kusalia nafasi ya saba ikiwa na alama 19 sawa na timu za JKT, Dodoma Jiji na KMC huku mashujaa ikiwa juu kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.