TIMU ya Green Warriors imeshuka daraja rasmi baada ya kupoteza mchezo wa leo kwa 3-2 dhidi ya Nyumbu ugenini kwenye mchezo wa Ligi ya First League.
Green imekusanya alama 11 kwenye michezo 14 iliyocheza ambazo hazikutosha kuwaweka salama kwenye ligi hiyo na hivyo kushuka hadi Ligi ya Mabingwa wa Mikoa kwa msimu wa 2026/27.
Nyumbu yenye alama 29 ilicheza michezo 14 ushindi nane, sare tano na kupoteza mchezo mmoja imeshika nafasi ya pili hivyo kukata tiketi ya kucheza hatua ya mtoano.
Cosmopolitan iliyopo nafasi ya tatu nayo itacheza hatua ya mtoano baada ya kufikisha alama 22 kwa kucheza michezo 14, ushindi michezo saba,sare moja na kufungwa michezo sita.
Moro Kids na timu ya Dar City zimesalia kucheza First League 2026/2027 baada ya kushika nafasi ya nne na tano kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Kwa upande wa Magnet na Pan African zitacheza michezo ya mchujo wa First League na timu zilizoshika nafasi ya sita na saba kutoka Kundi B.