JIBU la timu gani itaendelea kusalia ligi ya First League msimu wa 2025/2026 litapatikana leo Aprili 30 kwenye michezo ya mzunguko wa pili wa mtoano wa kushuka daraja (Relegation Play Off).
Mapinduzi itaialika Tunduru Korosho kwenye uwanja wa Nyamagana, Mwanza huku Magnet ikiwa mwenyeji wa Copco kwenye uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.
Kwenye michezo ya duru la kwanza Tunduru Korosho ilikuwa mwenyeji wa Mapinduzi kwenye uwanja wa Majimaji mkoani Songea mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 na Copco iliialika Magnet kwenye uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Timu zitakazopoteza katika matokeo ya jumla (aggregate) zitapata nafasi ya kuendelea kujitetea kwa kucheza na timu mbili zitakazoshika nafasi ya tatu na ya nne kwenye Fainali za mabingwa wa mikoa.