BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imepanga upya tarehe ya mchezo namba 180 wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/2024 kati ya Yanga na Simba maarufu kama ‘Kariakoo Derby’.
Mchezo huo ambao haukupangiwa tarehe kwenye ratiba iliyofanyiwa maboresho Februari 2024, sasa utachezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Aprili 20, 2024 kuanzia saa 11:00 jioni.
Klabu za Yanga na Simba pamoja na wadau wengine wa Ligi Kuu ya NBC wamepewa taarifa hiyo kuhusiana na mchezo huo na maandalizi yake yanaanza mara moja ili kuhakikisha unafanyika katika kiwango cha juu kinachoendana na hadhi ya michezo mikubwa ya Ligi ya sita kwa ubora barani Afrika.
Habari,naomba kujua utaratibu wa kupata gate pass mechi ya yanga na simba tarehe 20.