LIGI Kuu ya NBC inaendelea leo kwa mzunguko wa 23 kuanza rasmi katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya majira ya saa kumi alasiri.
Timu ya KenGold ndio mwenyeji wa mchezo huo ikiikaribisha timu ya Mashujaa kutoka Kigoma ambapo timu zote mbili zikitaka alama tatu muhimu.
KenGold iko nafasi ya 16 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa imekusanya alama 15 huku wakifunga mabao 18 na kuruhusu mabao 38 .
Mashujaa ipo nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa imekusanya alama 23 kufungaa mabao 17 na kuruhusu mabao 26.
Mchezaji wa kuchungwa katika mchezo huo wa kikosi cha KenGold ni Seleman Bwenzi akiwa amecheza michezo sita na kufunga mabao matano ikiwa ni mchezaji aliyeingia kwenye dirisha dogo la usajili.
Kwa upande wa Mahujaa mchezaji wa kuchungwa ni David Ulomi akiwa amefunga mabao manne.